Wanandoa
huwa na matarajio mengi sana katika maisha yao ya ndoa hasa matarajio mazuri
daima. Maisha ya ndoa ni mchakato ambao
hupita katika hatua kuu nne (4) yaani; kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Lakini
si ndoa zote hupitia hatua hizo zote nne (4) baadhi hupitia hatua tatu (3) au
mbili (2) kutokana na baadhi ya wanandoa kuacha kumkabidhi mlezi na mwanzilishi
wa ndoa duniani yaani; Mungu. Kwenye makala hii, sitaki kuongelea sababu anuai
zinazosababisha baadhi ya ndoa kutopitia hatua kuu nne (4) mzunguko wa maisha
ya ndoa. Baadhi ya matarajio maisha ya iliyo katika hatua ya pili (2) ni kama
yafuatavyo:-
ü
Changamoto
za masuala ya kifedha.
ü
Changamoto
zinazoletwa na wanandugu na watoto.
ü
Upweke.
ü
Kukua/kudumaa
kiroho.
ü
Migogoro.
ü
Magonjwa.
Kipengere
cha 4 hadi 7 nitavifafanua lakini cha 1 hadi 3 zilishavifanunua kwenye makala
zangu za awali za changangamoto zinazosababishwa
na wanandoa wenyewe na changamoto zinazosababishwa
watu wengine wasiyowanandoa.
Upweke; Kutokana na kuongezeka kwa
majukumu na uwajibikaji kwa masuala ya kifamilia maisha uliyokuwa unategemea
kuwa yatakuwa daima ya amani na furaha huanza kubadilika na hapo ndipo hali ya
kutaka kukaa kiupweke uanza kujitokeza ili kutafari zaidi majukumu ya kifamilia
na hamu ya tendo la ndoa hupungua kwa sababu ubongo unakuwa umezingirwa na
mawazo ya namna ya kutatua majukumu yaliyo mbele kama vile ada, kodi ya nyumba,
gharama za usafiri kwenda na kurudi kazini, chakula nakadhalika.
Migogoro; Kutokana ndoa kuwa katika hatua ya
kukua tabia zote zilizokuwa zimevichwa
na wanandoa wote uanza kudhihirika kwa sababu tabia haiwezi kufichwa daima.
Tabia za kiburi, jeuri, dharau, hasira, uasherati nakadhalika uanza kuonekana
na kuleta migogoro ya hapo pale katika ndoa. Hatua hii inahitaji busara na
hekima kubwa hasa kwa kumshirikisha Mungu, ili kuweza kuivuka na ndoa nyingi
sana huishia hatua hii.
Magonjwa; Kwa sababu za kimazingira na
vyakula imekuwa ni jambo la kawaida kwa binadamu kuugua kwa muda mrefu au
mfupi. Inapotokea uuguaji ni wa muda mrefu jambo ili uyumbisha sana hali ya uchumi
wa wanandoa na kama hakuna upendo wa dhati basi hata misingi ya ndoa uanza
kulegalega.
Mwacheni
Mungu awe mtawala katika maisha yenu ya ndoa kwa maana yeye ndie muasisi ya
taasisi ya ndoa hakika ndoa yenu itadumu na itakuwa kisima cha amani na furaha.
Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com
bure.
Jiunge na
blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA
MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.